MICHEZO NA BURUDANI
BADILI MFUMO WA MATUMIZI
Hali ya maisha sasa hivi imekuwa ni tofauti, makampuni yanabana matumizi hivyo nasisi lazima tubane matumizi. Hizi ni mbinu unazoweza kuzitumia kubana matumizi
1. Ukifanya maamuzi ya kuishi tafuta mahala ambapo ni karibu na ofisini kwako
2. Ukiwa ndani ya nyumba zima taa katika vyumba ambavyo havitumiki
3. Kama una mahusiano mazuri na wafanyakazi na mnakaa karibu wekeni mpango wa kutumia gari moja ili mchangie mafuta
4. Epuka kula nje ya nyumba ukiweza pika mwenyewe nyumbani.
5. Chagua harusi za kuchangia usichangie kila harusi kisa umeletewa kadi.
6. Badala ya kulipia channel 150 kwenye king'amuzi lipia channels unazoangalia tu
7. Badala ya kulipia gym jiunge na jogging clubs na fanya mazoezi mwenyewe (programs zipo kwenye internet)
8. Ukitoka out na mtu mwambie kuwa kila mtu atajilipia bili yake
9. Ukienda kazini toka na baadhi ya vyakula ambavyo mjini ni gharama au havipatikani kama matunda
10. Mtu akikuomba hela ghafla pima uzito wa maombi vinginevyo mwambie haiko kwenye bajeti mpaka utakapopanga bajeti nyingine.
11. Ukinunua taa nyumbani nunua zinazotumia umeme kidogo
12. Usipende kutembea usiku lolote linaweza likatokea likakugharimu pesa
13. Usipende kuazima kitu cha mtu kikipata tatizo huna namna zaidi ya kulipa wakati ambao hauna hiyo bajeti
14. Nguo unazoweza kufua nyumbani usipeleke dry cleaner.
15. Usisahau kuabudu na kumtolea Mungu Zaka na Sadaka
No comments:
Post a Comment