Monday, October 15, 2018

DEO H. FILIKUNJOMBE

DEO H. FILIKUNJOMBE




    
Deo Haule Filikunjombe (4 March 1972 – 15 October 2015) Alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la LUDEWA mkoani Njombe.

MH. Deo Haule Filikunjombe ni taa iliyozimika mapemakabla ya wakati wa kuzima kwake. Alikuwa bado anahitajika kwa wananchi wa Jimbo lake la Ludewa na kwa watanzania wote pia.

Wakati wa uhai wake alifanya mambo mengi sana kwa wananchi wake wa jimbo la ludewa na kwa watanzania.
Alishiriki katika miradi ya maji jimboni kwake (Madindo - mlangali)


Alishirikiana na wananchi katika jitihada za kuhakikisha umeme unafika jimboni kwake
Octoba 15 2015 taarifa ya majonzi ilitufikia kuhusu kifo cha mbunge wa Ludewa Deo Haule Filikunjombe na aliyekuwa Baba mzazi wa meya wa Ilala, William Silaa baada ya kupata ajali ya helikopta iliyoanguka katika mbuga ya Selous.

Vyombo mbalimbali vya habari viliripoti tukio hili la kusikitisha kwa wananchi
ITV walitufikishia taarifa hizi za kusikitisha namna hii.

Magazeti mbalimbali nchiniyalikuwahivi







    


Leo octoba 15 2018 watanzania tunakumbuka miaka mitatu ya kifo cha mbunge huyu kijana machachari nchini. Umuhimu wake kwa watanzania ulikuwa mkubwa mno, Watanzania wengi wataikumbuka michango yake mbalimbali ndani ya bunge na nje ya bunge.

Deo atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye sakata la ESCROW ambalo alilisimamia kwa kiasi kikubwa na kupeleka ripoti ya PAC bungeni akiwa na mwenzake ZITTO KABWE.
APUMZIKE KWA AMANI DEO HAULE FILIKUNJOMBE.

No comments:

Post a Comment